Victim photo

Stephano Mwasote

Hali: Aliuwawa Umri:

Wasifu:

Alipoonekana mwisho: Songwe

Stephano ni mwana wa Joseph Mwasote (maarufu kama China), Joseph ni mkazi wa Tunduma Songwe.Joseph anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana septemba 2025 mpaka leo haijulikani alipo. Oktoba 29 2025 Stephano aliandamana kama sehemu ya kudai haki ya baba yake.Akabeba bango lililoandikwa TUMECHOKA NA UTEKAJI, MRUDISHENI BABA YANGU. Jioni akarudi nyumbani salama. Oktoba 30 2025 akiwa nyumbani watu waliovalia kiraia wakiwa na silaha wakamfuata nyumbani na kumpiga risasi akafariki dunia.