John Isack Changawa
Wasifu:
Mkazi wa Iringa na Muhitimu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Shahada ya Sayansi na usimamizi wa Mazingira (B.Sc. ESM). Alihitimu mwaka 2021, baada ya kumaliza masomo alikua akijishughulisha na uuzaji na matengenezo ya simu. Ni mtu mcheshi, mkweli na mtu wa watu.
Alipoonekana mwisho: Iringa
Alichukuliwa na watu wasiojulikana tarahe 31/07/2025 maeneo ya maduka matatu Iringa mjini. Juhudi za kumtafuta zimefanyika tangu wakati huo mpaka sasa hakuwahi kupatikana. Katika juhudi za kumtafuta, zilizuka tetesi ameonekana Makao makuu ya polisi Dodom, lakini ndugu walipokwenda kuuliza polisi waliendelea kukana kuwa naye.